Frequently Asked Questions

Find answers to common questions about ViwandLink and our services.

Account 4 questions

Ninawezaje kujisajili kwenye ViwandaLink?

Kujisajili ni rahisi! Tembelea ukurasa wa Register kisha jaza taarifa zako zote muhimu. Baada ya kukamilisha, utapokea barua pepe ya kuthibitisha akaunti yako.

Je, kujisajili ni bure?

Ndiyo, kujisajili na kutumia ViwandaLink ni bure kabisa kwa watafuta kazi. Hakuna ada yoyote inayotozwa kwa ajili ya kutuma maombi ya kazi.

Ninawezaje kubadilisha password yangu?

Unaweza kubadilisha password yako kwa kwenda kwenye Dashboard yako, kisha bonyeza "Settings" au "Change Password". Utahitaji kuingiza password yako ya sasa na kisha password mpya.

Nimewahi kusahau password yangu. Nifanye nini?

Bonyeza Forgot Password kwenye ukurasa wa login. Kisha ingiza barua pepe yako na utapokea kiungo cha kuweka password mpya.

Jobs 4 questions

Ninawezaje kuomba kazi?

Tafuta kazi unayotaka kwenye ukurasa wa Jobs. Bonyeza kwenye kazi hiyo kwa maelezo kamili, kisha bonyeza kitufe cha "Apply Now". Hakikisha umekamilisha profile yako kabla ya kutuma maombi.

Je, ninaweza kuomba kazi nyingi kwa wakati mmoja?

Ndiyo, unaweza kuomba kazi nyingi tofauti kwa wakati mmoja. Hakuna kikomo cha idadi ya maombi unayoweza kutuma.

Nitaajuaje kama maombi yangu yamekubaliwa?

Utapokea arifa kwenye dashboard yako na barua pepe wakati mwajiri atakapopitia ombi lako. Unaweza pia kuangalia status ya maombi yako kwenye sehemu ya "My Applications".

Ninawezaje kuona kazi nilizozituma ombi?

Ingia kwenye dashboard yako, kisha bonyeza "My Applications" au "Maombi Yangu". Hapo utaona orodha ya kazi zote ulizotuma ombi pamoja na status zao.

Your Profile 4 questions

Ninawezaje kubadilisha taarifa zangu za profile?

Ingia kwenye dashboard yako, kisha bonyeza "My Profile" au "Profile Settings". Hapo unaweza kubadilisha taarifa zako za kibinafsi, elimu, uzoefu wa kazi, na mengineyo.

Je, ni taarifa gani muhimu ninazohitaji kujaza?

Taarifa muhimu ni pamoja na: jina kamili, barua pepe, namba ya simu, namba ya NIDA, namba ya TIN, kiwango cha elimu, uzoefu wa kazi, na CV/resume yako.

Ninawezaje kupakia CV yangu?

Nenda kwenye "My Profile" kisha tafuta sehemu ya "Upload CV" au "CV/Resume". Bonyeza kitufe cha kupakia faili, chagua faili yako (PDF, DOC, au DOCX), kisha bonyeza "Upload" au "Save".

Ninawezaje kupata Work ID yangu?

Baada ya akaunti yako kuthibitishwa na admin, system itakupa Work ID yako. Utapata arifa kwenye dashboard na barua pepe. Work ID yako itaonekana kwenye profile yako.

Verification 2 questions

Je, verification ya akaunti inachukua muda gani?

Verification inachukua kati ya siku 1 hadi 3 za kazi baada ya kuwasilisha taarifa zako zote muhimu. Utapokea barua pepe mara akaunti yako itakapothibitishwa.

Kwa nini akaunti yangu inahitaji kuthibitishwa?

Verification inasaidia kuhakikisha usalama wa mfumo na kuwa watumiaji wote ni halali. Hii inalinda waajiri na watafuta kazi dhidi ya ulaghai na taarifa bandia.

Technical Support 2 questions

Nina shida ya kuingia kwenye akaunti yangu. Nifanye nini?

Hakikisha unatumia barua pepe na password sahihi. Kama umesahau password, tumia "Forgot Password". Kama shida inaendelea, wasiliana nasi kwa email support@viwandalink.com au simu +255 712 345 678.

Ninawezaje kuripoti tatizo la kiufundi?

Wasiliana nasi kupitia ukurasa wa Contact au tuma barua pepe kwa technical@viwandalink.com. Tafadhali elezea tatizo lako kwa undani na uweke screenshot kama inawezekana.

Still have questions?

Contact us directly and our support team will be happy to help!

Contact Us